Bongo Movie

Video: Batulli kuajiri meneja ili kujibrand kimataifa na aeleza changamoto za msichana mrembo kufanya filamu

Yobnesh Yussuph aka Batulli ni miongoni mwa wasichana warembo kwenye kiwanda cha filamu Tanzania na weekend hii wakati wa uzinduzi wa filamu ya Lulu, Foolish Age tumepiga naye story kutaka kujua changamoto za msichana mrembo kama yeye kufanya filamu.

“Kwanza kila mtu anaamini kwamba una maisha mazuri,”anasema Batulli kuhusiana na changamoto za msichana mrembo kwenye filamu. “Kwahiyo kila mtu anahitaji msaada. Inawezekana nina maisha ambayo yananitosheleza mimi mwenyewe na familia lakini mtu wa nje hawezi kujua kwasababu watu wanapenda kuona mtu analia shida. Mimi sijazoea kulia shida, mimi naweza nikalala njaa nisikuambia sijala ili nifiche matatizo yangu.”

Katika hatua nyingine, Batulli amesema yupo kwenye hatua za mwisho za kuajiri meneja katika mikakati yake ya kujibrand kimataifa. “Naposema meneja simaanishi meneja tunakunywa naye pombe, hapana, by professional kabisa kila mtu atashangaa kwamba nawezaje kumlipa yule mtu.”

Ameongeza pia ili kujiweka vizuri zaidi ana mpango pia wa kurudi shule kuongeza elimu.

“Ili nifike mbali lazima nisome, lazima niongeze taaluma yangu,” alisema muigizaji huyo aliyeongeza kuwa hivi karibuni atafanya project na wasanii zaidi ya watano wa kimataifa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents