AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

VIDEO: Beyonce, Jay Z, Ed Sheeran na Tiwa Savage watikisa Afrika Kusini kwenye tamasha la Global Citizen

Siku ya jana Novemba 2 nchini Afrika Kusini kulikuwa na tamasha kubwa la burudani la Global Citizen, ambalo liliwakutanisha mastaa wakubwa duniani akiwemo Jay Z, Pharrel Williams, Beyonce, Usher na Ed Sheeran.

Beyonce na Jay Z walipanda wote jukwaani na walitumbuiza kwa takribani dakika 20, wengine walioamsha popo ni Pharrel Williams na Usher.

Maelfu ya watu walikusanyika Jumapili kwenye tamasha huko Johannesburg la kuenzi maisha ya Nelson Mandela nchini Afrika kusini.

Tamasha hilo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 tangu kuzaliwa kwa Rais wa kwanza mweusi wa Afrika kusini, Nelson Mandela na limefanyika jijini Johannesburg katika uwanja wa FNB.

Pia tamasha hilo limelenga kuelezea mapambano dhidi ya umaskini, ukosefu wa usawa wa kijinsia na njaa ambayo Nelson Mandela aliyapigania enzi za uhai wao.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW