Michezo

Video: Bifu zito la fukuta PSG, Neymar vs Cavani

Bifu zito lafukuta ndani ya klabu ya matajiri wa Ufaransa, Paris Saint-Germain baina ya mchezaji ghali zaidi duniani kwa sasa, Neymar da Silva Santos Junior  dhidi ya Edinson Roberto Cavani Gomez wote wakiwa wanakipiga katika timu hiyo.

Chanzo cha bifu hilo la Neymar  mwenye umri wa miaka 25, ambaye amenunuliwa kwa dau la paundi milioni 222 na kuweka rekodi ya dunia akitokea FC Barcelona dhidi ya Cavani kinatokana na mchezaji huyo wakimataifa wa Brazili kunyimwa nafasi ya kupiga penati katika mchezo wa PSG dhidi ya Lyon.

Kwamujibu wa mtangazaji wa L’Equipe, ameeleza kuwa kutofautiana kwa wachezaji hao wa PSG kuliendelea hata walipoingia Kwenyevyumba vya kubadilishia nguo hali iliyopelekea mchezaji, Thiago Silva kuingilia kati swala hilo.

https://youtu.be/aUbAjm6Zo-w

Muandishi huyo wa L’Equipe ameandika kuwa Neymar amechukizwa nakitendo alichofanyiwa ndani ya uwanja na mchezaji mwenzake kiasi ambacho walifikia hatua ya kusukumana ndani ya vyumba hivyo ndipo, Silva kuamua sakata hilo.

Kitendo cha Cavani kumsukuma Neymar kupiga adhabu ya penati ambayo PSG waliipata  dhidi ya Lyon kimeonekana kama sio kitendo kizuri machoni mwa watu jambo ambalo ameonekana kuwahi kufanya hivyo hata hapo kabla.

Kiongozi wa klabu hiyo hakufurahishwa na kitendo kilichofanywa na Cavani kiasi kwamba kuamua sikuchache zijazo mchezaji  sahihi atakeyeruhusiwa kupiga adhabu ya mikwaju ya penati pale itakapo tokea ndani ya kikosi cha Paris Saint-Germain.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents