Habari

VIDEO: Bodaboda 20 wakamatwa na Polisi Dar kwa tuhuma za kushambulia kwa mawe Basi la Mwendokasi

Madereva Bodaboda 20 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa tuhuma za kushambulia kwa mawe na kuharibu basi la Mwendokasi wiki iliyopita.

Bodaboda hao wanadaiwa kulishambulia basi hilo, baada ya mwenzao kugongwa na kufariki dunia Jumamosi iliyopita Desemba 8 Usiku.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jumanne Desemba 11, 2018 Kamanda wa Kanda ya Dar Es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema Desemba 8, saa mbili usiku eneo la Manzese Tiptop, dereva bodaboda mmoja akiwa anapita katika barabara ya mwendokasi aliligonga basi hilo na kusababisha vifo vya watu wawili ambao walikuwa wamepakiwa Mishikaki na kisha dereva wa bodaboda hiyo (Yenye Namba MC  964 BYN ) kufariki muda mfupi baada ya kupelekwa Hospitali.

Kwa upande mwingine, Kamanda Mambosasa ametoa onyo kali kwa madereva wote wa vyombo vya moto hususani badaboda kuacha mara moja kutumia barabara za mabasi ya mwendokasi ili kuepusha ajali kama hizo.

Kila mmoja aheshimu sheria za nchi,  hatutaacha kuchukua hatua kwa yeyote ambaye ataendelea kufanya uhalifu huo wa matumizi mabaya ya barabara na kusababisha ajali ya namna hiyo,“amesema Mambosasa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents