Videos

Video: Bongo Star Search 2013 yazinduliwa rasmi leo

Shindano la kusaka vipaji vya uimbaji muziki la Epiq Bongo Star Search, EBSS, leo limezinduliwa rasmi jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo uliofanyika makao makuu ya Zantel umehudhuriwa na Mkurugenzi wa Benchmark Production, Rita Paulsen a.k.a Madam Rita ambaye ni mwanzilishi na mmoja wa majaji shindano hilo, Afisa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan pamoja mshindi wa shindano hilo mwaka jana, Walter Chilambo.

Mwaka huu, EBSS ambayo itajulikana kwa kauli mbiu ya ‘KAMUA’ itaenda kufanya usaili kwenye mikoa sita ya Mbeya, Arusha, Zanzibar, Mwanza, Dodoma na Dar es Salaam.

Usaili utaanzia Dodoma tarehe 29 and 30 ya mwezi huu katika ukumbi wa Maisha Club, ikifuatiwa na Zanzibar tarehe 5 na 6 mwezi wa saba katika hoteli ya Bwawani. Mbeya usaili utakuwa tarehe 10 hadi 11 mwezi wa saba pale club Vybes, Mwanza tarehe 14 hadi15 mwezi wa saba Club Fussion, na Arusha itakuwa tarehe 20 hadi 21 mwezi wa saba Club Tripple A ikimalizikia na Dar es Salaam tarehe 26 hadi 28 pale Uwanja wa Taifa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents