Michezo

Video: Chelsea bingwa EPL 2017

Klabu ya Chelsea wakicheza ugenini wamechukua ubingwa wa Ligi Kuu ya England baada ya kupata ushindi wa 0-1 dhidi ya West Brom.

https://youtu.be/oGS2o207Gm0

Goli pekee lililoipa ushindi Chelsea lilifungwa na Michy Batshuayi katika dakika ya 82.

Chelsea wakicheza ugenini wamechukua ubingwa wa Ligi Kuu ya England baada ya kupata ushindi wa 0-1 dhidi ya West Brom.

Tottenham ambao ndio waliokuwa wapinzani wa karibu wa Chelsea katika nafasi ya pili, walipoteza mchezo wao dhidi ya West Ham Mei 5, na hivyo kuifanya Chelsea kuhitaji kushinda mechi mbili kati ya nne zilizosalia.

Walishinda mechi yao dhidi ya Middlesbrough 3-0 Jumatatu Mei 8, na kukamilisha pointi walizohitaji kuchukua ubingwa kwa kuizaba West Brom siku ya Ijumaa Mei 12.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents