Habari

Video: CNN wamepata video inayoonesha jinsi shambulio la Westgate lilivyoanza, itazame

CNN wamepata video nyingine inayoonesha jinsi tukio la kuvamiwa kwa Westgate Kenya (September 21) lilivyoanza.

Video hiyo iliyochukuliwa kwa camera za ndani ya jengo (CCTV) inaonesha hali ilivyokuwa kabla ya shambulio kuanza siku ya kwanza, wateja walikuwa wanaendelea na shughuli mbalimbali karibia na lango kuu la kuingilia ndani ya mall, ghafla kila mtu alianza kukimbia kuokoa maisha yake huku wengine wakilala chini.

Sehemu ya Video hiyo inaonesha wakati watu wakikimbia ndipo gaidi mmoja alitokea na kumpiga risasi mtu aliyekuwa amejisalimisha kwa kulala chini mbele yake, mtu huyo aliyejeruhiwa alijaribu kunyanyuka lakini gaidi huyo alirudi na kummalizia kwa risasi.

Tazama video hiyo hapo juu

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents