Habari

Video: CUF upande wa Lipumba waomba radhi wapiga kura wao

Chama cha Wananchi(CUF), upande wa Profesa  Ibrahim  Lipumba anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya siasa nchini  wamewaomba radhi wapiga kura wa jimbo la Kinondoni  baada ya aliyekuwa mbunge  wa jimbo hilo kupitia chama hicho, Maulid Mtulia kujiuzulu kwa kile alichodai anaunga mkono juhudi za Rais Magufuli.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Makao Makuu ya chama hicho Buguruni,  Mkurugenzi  wa Habari, Uenezi na Mawasiliano ya Umma, Abdul  Kambaya amesema Chama hicho hakikutarajia kuingia katika uchaguzi mdogo hasa jimbo la Kinondoni  kabla ya Uchaguzi Mkuu.

“CUF  haikutarajia kuingia katika uchaguzi mdogo hasa jimbo la Kinondoni  kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 labda kingetokea kifo. Tunawaomba radhi wakazi wa Kinondoni,” amesema Kambaya.

Aidha amesema kuwa  CUF iliwaaminisha wakazi wa Kinondoni  kwa kumpeleka Mtulia kugombea jimbo hilo kwa kuwa ni mtu makini.

Disemba 2 mwaka huu, Mtulia alitangaza kujiuzulu nafasi ya zot za uongozi ndani ya chama hicho na kujivua uanachama.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents