AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Video: Cyrill Kamikaze aeleza kwanini anaogopa kuingia kwenye ndoa

Rapper Cyrill aka Kamikaze amefunguka kuwa akijiangalia kwa sasa hajioni kama yuko tayari kuingia kwenye ndoa kwakuwa hilo si jambo la mzaha.

Akiongea juzi kwenye kipindi cha Pillow Talk cha Times FM, Cyril amesema haogopi kuingia kwenye ndoa kwa sasa si kwakuwa anaogopa majukumu bali ni ngumu kumpata mchumba mwenye sifa za kuwa mke.

“Tunafuata mara nyingi uzuri wa mtu unapotafuta mwanamke. Sasa kwenye ndoa uzuri unapotea. Utaamka utakuta chai mezani? Au utaamka wewe kwenda kutengeneza chai? Naamisha zile mutual understanding, feelings ziendane, ” alisema Kamikaze.

Cyrill amesema ili kupata mwanamke wa kuoa inabidi umfahamu mtu vizuri na kwa muda mrefu kwakuwa ni rahisi mpenzi wako kuigiza kabla ya kuingia kwenye ndoa.

“Kwasababu ndoa mnaenda kuishi under one roof, na uchumba mara nyingi sio one roof, wewe una ghetto lako mimi nina ghetto langu tunakutana kwa masaa masaa sasa ile kujitune ni rahisi.”

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW