AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

VIDEO: Diamond amtolea ya moyoni Hamisa Mobetto kupitia wimbo mpya ‘KATIKA’ wa Navy Kenzo

Kundi la Navy Kenzo limeachia club banger nyingine mpya inayokwenda kwa jina la Katika wakiwa wamemshirikisha Diamond Platnumz.

Habari kubwa kwenye hiyo ngoma sio tu kwa sababu ni ngoma kali, bali ni mistari inayopatikana kwenye mkwaju huo sana sana lyrics za Diamond Platnumz ambaye amekiri kuwa kwa sasa uchawi wa mzazi mwenzie Hamisa Mobetto umemuingia haswaa.

Diamond amesikika akiimba “Na kalivyo na body kinanda, Sepetu. Tunguli zimenibamba Mobetto” mstari ambao watu wengi wameutafsiri kama ni attention ya kutaka wimbo uzungumziwe.

Wiki tatu zilizopita Diamond na Mobetto waliingia kwenye vita ya maneno, baada ya kuvuja kwa sauti ya Mobetto mitandaoni ikisikika akiongea na mtu aliyedaiwa kuwa ni Sheikh akitaka amsomee duwa ili aolewe.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW