Burudani

Video: Diamond ana-inspire vijana wengi -Rio Paul

Mbunifu wa mavazi kutoka Tanzania, Rio Paul amesema kuwa Diamond Platnumz amekuwa na mtu mwenye ushawishi mkubwa kwa vijana wa sasa katika suala la maendeleo.

Akiongea na Bongo5, Rio ambaye pia ni Balozi wa vijana amesema yeye kama mjasiliamali ana mkubali Diamond kwani ni mjasiliamali anayefanya vizuri katika muziki na biashara na amekuwa mtu mwenye ushawishi hasa kwa vijana.

“Nimekuja kujumuika na watu mbalimbali kujifunza mambo mengi, ukiangalia Diamond sio tu mwanamuziki ila pia ni mjasiliamali na amekuwa ana-inspire vijana wengi na amekuwa balozi wa Belaire, hivi karibuni na amefanya mambo mbalimbali ya maendeleo na anatufanya sisi vijana wenzake waTanzania tuwe inspired,” amesema Rio.

Akaongeza ” Cha msingi ni sisi vijana tupigane kufika alipofika na tupeperusha bendera ya nchi yetu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents