Michezo

Video: Dismas Ten apata tetesi watani zao Simba kuishangilia Yanga SC Jumamosi

Msemaji wa klabu ya Yanga, Dismas Ten kupitia mkutano wake na waandishi wa habari hii leo amesema kuwa amesikia Simba hapo kesho watakwenda kuwashangilia watakapo kuwa uwanjani dhidi ya Azam FC.

 

“Tumesikia Simba kesho watakuja kutushangilia, niseme tu hii si mara ya kwanza wao kutushangilia, wameshatushangilia mara nyingi, ni jambo jema, sisi ni watani wa jadi na hakuna uadui kati yetu.”amesema Ten

Dismas Ten ameongeza “Tunawakaribisha kwani mpira wa miguu ni mchezo wa kiungwana, hakuna jambo baya, tunawashukuru kwa kujitolea kwao.”

Simba wataungana na mashabiki wa Yanga SC katika kuishangilia ili timu ya Azam FC iweze kupoteza katika mchezo huo na wao waweze kujikita zaidi kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Vodacom.

Mpaka sasa Simba inaongoza katika msimamo wa ligi kwakuwa na jumla ya pointi 32, wakati Azam ikiwa na katika nafasi ya pili kwa kuwa na alama 30 na Yanga  na 25.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents