Habari

Video: Dkt Shein aisifu kampeni ya Mimi na Wewe iliyoanzishwa na RC Ayoub

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Ali Mohamed Shein amemsifu Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohamed Mahamoud kwa kuanzisha kampeni ya Mimi na Wewe ambayo imesidia wakazi wa Mkoa huo ikiwemo kujenga shule ya Msingi, Kijitopele kwa siku 11, shule ambayo ilitelekezwa kwa zaidi ya miaka mitano bila kuendelezwa.

Hata hivyo Rais Shein, alitoa maagizo kwa viongozi hao kuhakikisha  wanafanya usimamizi mzuri wa kazi kwa kutoa elimu kuhusu suala zima la ukimwi ikiwemo kwa wamama wajawazito na kuongeza juhudi za uchangiaji damu, kuongeza idadi ya walimu katika shule hasa walimu wa kiume amabo wamonekana kuwa wachache mashuleni.

Katika kukomesha migogoro ya ardhi, Dkt Shein amewataka kuwafichua viongozi wote wanaohusika kuuza ardhi kinyemela na kusababisha mtafauruku kubainisha na kutoa majina yao kwake ili aweze kuwachukulia hatua kali.

Na Laila Sued na Salum Kaorata

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents