Burudani ya Michezo Live

Video: Exclusive Interview na Hisia (TPF6)

Mwakilishi wa Tanzania kwenye shindano la Tusker Project Fame msimu wa sita, Elisha Hisia aliongea na Bongo5TV kuelezea shindano hilo na kudai kuwa hakutegemea kama angeshika nafasi ya nne.

Kwenye mahojiano hayo, Hisia alisema Watanzania wameonesha support ya nguvu kwake kwa kumpigia kura kwa wingi.

“Sikutegemea kushika namba 4,” alisema. “Nilitegemea kushinda kwasababu japokuwa tulikuwa ndani kule na hatujui vitu vingi vinavyoendelea nje maana tulikuwa hatuna mawasiliano lakini support ilikuwa nzuri, tumewakilisha Tanzania ipasavyo. Watu walikuwa wanapiga kura, mtu yeyote anayesema watanzania walikuwa hawapigi kura sio mwaka huu, mwaka huu Watanzania wamepiga kura. Nimetoka nje nimekuja kuona kuna watu walikuwa na accounts sijui 10, wanapiga kura atleast 200 kwa siku. Mtu ile meseji 40 kwa siku anaweka 6000, mtu anaweka 6000 kwa siku ili ampige kura Hisia, mtu hata simfahamu. Kwahiyo sikutegemea kuwa wanne.”

Ushindi wa TPF6 ulienda kwa mshiriki wa Burundi, Hope.

Katika hatua nyingine Hisia alisema wimbo wake mpya uitwao Kwaajili Yako, aliuandikia huko huko Kenya na sio wimbo aliokuwa amepanga kuurekodi. Anasema kuna matatizo yalitokea na kufanya asiufanye wimbo aliokuwa arekodi na hivyo kumfanya producer Eric Musyoka amsikilizishe beat zingine na kuchagua moja ambayo aliitumua kuandika wimbo huo.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW