Michezo

Video: Fainali yauwa watu Senegal

Mashabiki wanane wamefariki dunia uwanjani na wengine zaidi ya 90 kujeruhiwa baada ya kuangukiwa na ukuta wakati wakiruka ili kujiokoa kwenye vurugu zilizotokea uwanjani nchini Senegal siku ya Jumamosi.

Mashabiki wa mpira wa miguu nchini Senegal wakikimbia kutokana na vurugu zilizo zuka Uwanjani katika mchezo wa Stade de Mbour dhidi ya Union Sportive Quakam

Vurugu hizo ziliibuka wakati wa mechi ya fainali Kombe la Ligi iliyozikutanisha klabu za Stade de Mbour na Union Sportive Quakam katika uwanja wa Demba Diop uliopo Dakar.

Mapigano yaliibuka uwanjani baina ya mashabiki na polisi na walinda usalama hao walijibu kwa kuwarushia maji ya kuwasha pamoja na mabomu ya machozi, jambo lililoongeza ghadhabu kwa mashabiki hao na wengine kujiokoa kwa kuruka ukuta.

Mpaka dakika 90 timu hizo zilifungana mabao 1-1 na katika muda wa nyongeza Mbour walikuwa wa kwanza kupata bao na kufanya matokeo kuwa 2-1, jambo lililosababisja kuibuka kwa vurugu kutokana na wapinzani wao kugomea bao hilo.

Cheikh Maba Diop ambaye rafiki zake ni miongoni mwa watu waliofariki katika ajali hiyo wakati walipo jaribu kuwasaidia wenzao kutoka nje ya uwanaja huo amekiambia chombo cha habari cha AFP  kuwa ilitokea khafla mara baada ya ukuta kuanguka.

“Iilikuwa tukio la khafla mara baada ya ukuta ulipoanguka, tulifahamu wazi kuwa wapo miongoni mwetu wamefariki kwa sababu ukuta uliangukia watu moja kwa moja” amesema Cheikh Maba .

https://youtu.be/P8r02qR52nE

By Hamza fumo

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents