Bongo MovieBurudani

Video: Filamu ya ‘Tunu’ itabadili mtazamo mmbaya kuhusu Bongo Movie – JB

Msanii wa filamu nchini, Jacob Stephan ‘JB’, ambaye ni mmoja kati ya wasanii wa filamu alioigiza ndani ya filamu mpya ya ”Kumekucha Tunu’. Amedai filamu hiyo ni moja kati ya filamu ambazo zimeandaliwa nchini Tanzania kwa kushirikiana na madirector wa nje, ili kupata kitu kipya ambacho kitabadili mtazamo wa watu kuhusu Bongo Movie.

Filamu hiyo imeongozwa na mtoto wa muongozaji mkongwe wa filamu, ambaye aliongoza filamu ya ‘Neria’, ambayo ilifanya vizuri barani Afrika na Duniani.

Akiongea na waandishi wa habari akiwa katika uzinduzi, ndani ya ukumbi wa Sinema wa Quality Center (Sineplex Suncrest Cinema), JB alisema filamu hiyo itawafungua macho mashabiki ambao wamekuwa wakiitupia madongo tasnia hiyo.

“Katika hii movie kuna mambo mengi humu ndani, kuna mapenzi, ugomvi na kwa ujumla ni filamu ya kuelimisha jamii kuhusu kilimo. Ndani ina mikasa mingi ya kusisimua. Mimi wakati naambiwa bwana JB tunataka uigize kwenye hii filamu yetu sikujiuliza mara mbilimbli, hata pesa sikuuliza nitalipwa shilingi ngapi, kwa sababu ya ukubwa wa hii project, nilitaka niwepo ndani niangalie wenzangu wanafanya nini na nipate kujifunza,” alisema JB.

Aliongeza, “Kwa hiyo wakati tunalalamika kuhusu kuibiwa kazi zetu na sisi wasanii tunatakiwa kukaza zaidi, ili kuwanyima nafasi wale mashabiki ambao wanakosoa filamu zetu, kwa sababu lisemwalo lipo kwa hiyo sisi kama wasanii ni jukumu letu kufanya kazi kwa bidii tuboreshe tasnia yetu,”

Katika hatua nyingine muigizaji huyo amedai baada ya kutokea kwenye filamu hiyo, alipata fursa ya kupewa mafunzo ya kuongoza filamu kwa kuwa ni kazi ambayo anaenda kuifanya baada ya kustaafu kuigiza.

“Namshukuru Mungu filamu hii pia imenipa nafasi ya kujifunza vitu vipya kwa sababu mimi nimebakiza filamu moja nistaafu. Kwa hiyo baada ya kumaliza kuigiza filamu yule muongozaji akaniuliza baada hapa una plan gani katika maisha yako, nikamwambia kwa sasa nakimbilia miaka 40 nataka kuacha kuigiza nibaki kama director akafurahi sana, akanipatia mafunzo ya wiki mbili na baada ya hapo akanipa kazi ya kuongoza filamu nilishirikiana naye ambayo pia itatoka hivi karibuni kwahiyo kwangu mimi hii ni nafasi nzuri sana,”

Filamu ‘Kumekucha Tunu’ itakuwa inaonyeshwa kwenye kumbi mbalimbali za sinema hapa Jijini Dar es salaam.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents