Michezo

Video: Floyd Mayweather ashtakiwa na ex wake Shantel Jackson

Bondia Floyd Mayweather ameendelea kuwa kwenye headlines kwa scandal nyingine tena wiki hii. Mpenzi wake wa zamani Shantel Jackson, anamshtaki kwa madai kuwa alimshambulia mara kadhaa ikiwa pamoja na kumwekea bunduki kichwani kwake kumtishia kumuua.

Kwa mujibu wa nyaraka za kisheria ambazo TMZ wanazo, Jackson anadai kuwa Mayweather alianza kumpiga mwaka 2012, baada tu ya kutoka jela alikofungwa kwa kumshambulia mwanamke mwingine. Jackson anadai pia kuwa Mayweather alimuuliza tena April 2013 kwa kuukunja mkono wake na kumnyooshea bunduki kwenye mguu wake na kuumuuliza kidole kipi anataka akipige kwa risasi!

Kwa ujumla Shantel Jackson anamshtaki Mayweather kwa kumshambulia, kumchafua, kuingia masuala yake ya faragha, kumkosesha raha kwa makusudi, kumsumbua na makosa mengine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents