Habari

Video: Foleni ya magari yauwa watu 12

Watu 12 wamefariki nchini Indonesia kutokana na foleni ya magari iliyosababisha mamilioni ya watu kukwama barabarani siku kadha.
giant-traffic-jam

Wengi walifariki kutokana na kukosa maji mwilini na uchovu.

Watu wengi waliokuwa wakisafiri kwa sherehe za kuadhimisha mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhan walikusanyika katika makutano ya barabara kisiwa cha Java.

Na hapo ndipo msongamano mkubwa wa magari ulipotokea.

Maafisa wa uchukuzi nchini Indonesia wanasema vifo hivyo vimetokea katika kipindi cha siku tatu
.
Vyombo vya habari nchini Indonesia vinasema wengi wa waliofariki ni wazee ambao walikwama ndani ya magari chini ya joto kali.

Mtoto mmoja mchanga alifariki kutokana na kinachodhaniwa kuwa ni kupumua hewa chafu iliyojaa moshi wa magari.

https://youtu.be/Bz7WseVbFnk

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents