Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Video: Foleni ya Ujerumani inavyomfanya kijana kuogelea km 2 kuwahi kazini

Umeshawahi kutafakari njia mbada ya usafiri ambayo inaweza kukufikisha kazini mapema? Benjamin David kutoka mjini Munich, Ujerumani ameamua kuvumbua njia yake mpya ambayo inaweza kumfikisha kazini kiurahisi.

Benjamin ameamua kuutumia mto Isra ambao up karibu na maeneo anayoishi ili kuweza kuwahi kazini kutokana na foleni nyingi za mjini humo. Kijana huyo huogelea kila siku katika mto huo kwa urefu wa kilomita mbili ii kuweza kuwahi kazini kwake.

Akiongea na BBC, Benjamin amefunguka sababu ya kuchukua maamuzi hayo, “Foleni ya magari karibu na mto Isar huwa mbaya sana. Ninapokuwa naogelea huwa nasonga kwa kasi zaidi na huwa nimetulia zaidi.”

Mwanamume anayeogelea kwenda kazini

Mwanamume huyu huogelea kwenda kazini ili kukwepa foleni.Wewe unaweza?#bbcswahili #munich #isar #foleni

Posted by BBC Swahili on Sunday, August 6, 2017

Katika kuhakikisha vitu vyake vinakuwa salama pindi anapoogelea Benja ana mfuko maalum ambao unakinga vitu vyake visiharibike na maji. “Nina kitu hiki kizuri sana ambacho kilivumbuliwa na kijana mmoja Basel, alijiuliza swali sawa na nililojiuliza. Nitawezaje kufika kazini nikiwa nimekauka? Hii haipenyezi maji na ninaweza kuweka vitu vyangu vyote ndani. Kwa kuifunga inatanuka na kuwa kama boya ambalo linaloweza kuelea,” ameongeza.

Ameendelea kwa kusema, “Wazo hili lilinijia kwani mto Isra ulikuwa ukitumiwa kwa uchukuzi kwa zaidi ya miaka 150. Ilikuwa ni njia kuu za uchukuzi kusema ukweli kati ya Roma na Vienna. Watu walitumia mitumbwi mto Isra, lakini hili limetoweka katika kipidi cha miaka 100 iliyopita. Hakuna anayetumia Isra kwa uchukuzi tena ila ni mimi peke yangu. Sitashangaa miaka ijayo watu wakianza kuutumia zaidi mto Isra kwa usafiri asubuhi.”

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW