Tupo Nawe

Video: Harmonize aongea Kimakonde jukwaani, mashabiki wamuunga mkono

Wakati wasanii mbalimbali wakifanya mazoezi ya mwisho jukwaani kabla ya kuanza kwa tamasha la WasafiFestival hii leo Novemba 24 mwaka 2018, Harmonize alitumia nafasi hiyo kuzungumza lugha ya Kimakonde na mashabiki zake ambao wameonyesha kumuunga mkono kutokana na kufahamu kile kinachozungumzwa.

Harmonize ambaye ni msanii kutoka kundi la WCB, yeye ni mwenyeji wa Mtwara mahala ambapo ndipo alipotokea hivyo kuzungumza lugha ya Kimakonde ni kawaida kutokana na wakazi wa Mkoa huo kutumia kama sehemu ya mawasiliano.

Tamasha la WasafiFestival linazinduliwa rasmi mkoani Mtwara huku jumla ya wasanii 36 wakitarajiwa kufanya ‘show’ show usiku wa leo wakiwemo wenyewe WCB.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW