Burudani

Video: Hawa ndio wasanii wawili wakubwa ambao Nemo anatamani kufanya nao kazi

Nemo amewataja wasanii wawili ambao anatamani kufanya nao kazi.

Akiongea na Bongo5, msanii huyo ambaye Jumatatu hii ameachia wimbo wake mpya ‘Kipotabo’ baada ya kimya cha miaka mingi, amewataja wasanii hao kuwa ni Ben Pol na Chris Brown kwa Marekani.

“Mbele mara nyingi nilikuwa na ndoto za kufanya kazi na Chris Brown. Muda mwingi utakuta ndio role model wangu nikisikiliza ngoma zake, nikiimba ngoma zake nyingi. Kwa Bongo ningependa kufanya kazi na Ben Pol, achana tu ni mshikaji wangu nadhani pia kile ninachokifanya mimi anaweza kukimudu kwa wakati wa karibu ingawaje wapo wengi ambao ningependa kufanya nao kazi kwa vizuri.

“Lakini kwa Ben Polanaweza kukifanya ninachokifanya mimi anaweza akawa na utayari wa ukaribu zaidi wa kufanya hicho kitu kwa hamu zote,” ameongeza. Kwa sasa msanii huyo yupo chini ya lebo mpya iitwayo Digital City Drimz.

Hii ndio video ya wimbo mpya wa Nemo, Kipotabo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents