Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Video: Hii ndio mipango ya Akon kuinua muziki wa Afrika

Msanii wa Marekani mwenye asili ya nchini Senegal, Akon amefunguka mipango yake ya kusaidia zaidi muziki wa Afrika kuweza kukuwa duniani.

Akiongea na shirika la habari la BBC, msanii huyo amesema, kwa sasa anamipang ya kuanzisha mtandao utakaofahamika kama ‘Musik Bi’ ambao pia utaweza kuonyesha ni jinsi gani muziki wa Afrika unavyozidi kukuwa tofauti na ilivyokuwa hivi sasa inakuwa ngumu kuonekana ukuaji wake.

“Nyimbo nyingi zitakuwa ni kutoka Senegal, lakini lengo langu ni kutoa huduma pia nje ya mipaka ya Senegal kwa ujumla kusambaza muziki wako, kununua muziki na kupata muziki kutoka kwenye mtandao,” amesema Akon.

Akon ana mipango mikubwa kuhusu muziki Afrika

Akon ana mipango mikubwa kuhusu muziki Afrika 🎼🎹🎵

Posted by BBC Swahili on Wednesday, August 30, 2017

“Huenda biashara ya burudani imekuwa zaidi Afrika kuliko ilivyo Marekani lakini huwezi kuibaini tofauti hii kwa sababu hakuna rekodi yake au takwimu kwani ni biashara inayotumia pesa taslimu Afrika. Kulingana na mimi naona kunathamani Afrika sioni kwa nini unahatarisha maisha yako kuvuka ng’ambo wakati unaweza kupata zaidi ukiwa Afrika. Kwa hiyo tunajaribu kuwahamasisha kuzingatia kuwekeza barani Afrika na kujenga Afrika inavyostahili kujengwa,” ameongeza.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW