Habari

Video: Hotuba ya Rais Kikwete kwenye mazishi ya Mandela

Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete kwenye mazishi ya Rais wa kwanza wa Afrika Kusini Nelson Mandela leo huko Qunu, Eastern Cape nchini Afrika Kusini, imewakumbusha Waafrika ukaribu wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Afrika Kusini.

Katika hotuba hiyo iliyosifiwa na Waafrika wengi, Kikwete aligusia jinsi ambavyo Afrika Kusini haipo peke yake kwenye maombolezo ya shujaa wao, Mandela.

“Watu wa Tanzania wangependa mjue kuwa hamko peke yenu. Watakuwa nanyi katika kipindi hiki cha maombolezo na baada ya hapa. Potezo lenu ni potezo letu. Alikuwa kiongozi wetu, shujaa wetu, mfano wetu, baba yatu kama alivyo kwenu. Watu wa Tanzania wamepoteza rafiki mkubwa. Komredi mkubwa jeshi,” alisema Kikwete.

Katika hotuba hiyo pia, Kikwete alikumbushia jinsi Nelson Mandela alivyoacha viatu vyake jijini Dar es Salaam mwaka 1962 ambavyo vilirudishwa kwake alipokuja kuwa rais. Ulikuwa ni muendelezo mwingine wa kuvutia wa ujio wake Tanzania mwaka 1962,” alisema.

“Katika kuufanya ujio wake kuwa makini, hakukaa kwenye hoteli. Alikaa kwenye nyumba ya Cyril Swai. Alipoondoka, aliacha viatu vyake kwa matumaini kuwa akiwa anarudi angevipitia viatu vyake Bahati mbaya hakupitia Dar es Salaam tena sababu aliporejea Afrika Kusini alikamatwa na kukaa jela miaka 27. Bahati nzuri, familia ya Swai ilivitunza viatu vyake na mwaka 1995, viatu hivyo vilirudishwa kwake.”

Mjane wa Swai, Vicky alikuwepo pia kwenye mazishi ya Mandela.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents