Soka saa 24!

Video: Humud aapa kwa uongozi wa KMC ‘Nitaweka wazi kashifa zao, nitakuwa kama Dudu Baya Konki Master, nipo tayari kufa

Aliyekuwa mchezaji wa klabu ya Manispaa ya Kinondoni KMC, Abdulhalim Humud maarufu kama ‘Gaucho’ mara baada ya kukutana na waandishi wa habari na kukanusha taarifa za kuhusika na utovu wa nidhamu ikiwemo kuwasumbua wake wa wachezaji wenzake ndani na nje ya uwanja taarifa zilizotolewa na timu yake hapo jana amewataka mabosi wake wa zamani kuwacha kumchafua na endapo atasikia akichafuliwa tena na yeye hatowafichia kashifa zao kubwa walizonazo.

”Bila kuwa imara mkewangu kwa kipindi hiki hapa pengine ningekuwa tofauti naye, sasa hili ambalo wao walilitaka siyo sahihi,” amesema Humud

Abdulhalim Humud ameongeza kuwa ”Wao sasa hivi wameshanipakazia mimi vitu vyaajabu ambavyo siyo vya ukweli, wamekaa na familia zao wametulia, maisha yao na familia zao yanakwenda mimi naanza kuangaika na familia naanza kupigiwa simu kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki wakizungumza vitu vya tofauti tofauti.”

”Hatakama naonekana sina nidhamu  hii siyo hatua am,bayo mimi walitakiwa kunifikishia, tusifikie hatua ya vile vizuri ndiyo tun avipiga vita.”

”Kuna jambo nataka nilizungumze ambalo meneja wangu, mke wangu na watu wangu wa karibu ambao wamekuwa wakinisapoti kwenye matatizo mbalimbali yanayo ni kabili wamekuwa wakinizuiya nisi yazungumze, nilitaka kuyazungumza lakini wameniambia nisiseme.”

”Na nilifikiri ingekuwa sahihi kwasababu wao viongozi wa KMC wameamua kunichafua ilibidi na mimi sasa niwachafue lakini kwa heshima na ubinadamu na kulinda soka letu la Tanzania kunabaadhi ya mambo mimi siwezi kuyazungumza.”

”Na siyazungumzi si kwamba nawaogopa viongozi wa KMC, hayo ambayo sitaki kuyazungumza ni miongoni mwa kashifa ambazo siyo sahihi  ujue ndiyomaana hata Dudu Bayaya kilasiku unamsikia anasema Konki Konki Konki Master akiwa anamaana, kwa hatua waliyonifikishia na mimi nilikuwa natakiwa kuwa kama Dudu Baya anavyo kuwa lakini kwasababu ya faida ya mpira wa Tanzania siwezi kufanya hivyo.”

”Humud amewashukuru mashabiki zake kwa kuhakikisha wanakuwapamoja naye bila kumsahau meneja wake na mkewe huku akiahidi kuwa iwapo atasikia kitu kingine chochote cha kashifa kuhusu yeye kikitokea KMC na kukubali yeye kuwafichia kashifa zao basi atakuwa tayari kufa ama kwenda jela lakini ataziweka kashifa zao ambazo ni kubwa bila kujali yeye ataishia wapi.”

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW