Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Video: Huyu ndio msanii wa Afrika Mashariki aliyeamua kumtumia mpenzi wake kwenye video yake

Ni mara chache tumeona wasanii wa muziki wakiwatumia wapenzi wao kama model kwenye video za ngoma zao. Sasa msanii wa Burundi Daddy Face ameamua kumtumia mpenzi wake kama model kwenye video ya wimbo wake mpya ‘Marry Me’.


Daddy Face akiwa na mpenzi wake wakiwa location wanashoot video

Kitu hicho tumeweza kukiona kwa Diamond alipomtumia Zari kwenye ‘Utanipenda’, Jux alimtumia Vanessa Mdee kwenye video yake ‘Sisikii’, Barnaba na Mama Steve kwenye ‘Wahale’ na nyingine chache.

Msanii huyo wa Burundi ambaye anaishi nchini Marekani ameamua kufanya hivyo kwa madai kuwa anataka kuwaonyesha watu ni kiasi gani anavyompenda mpenzi wake huyo ambaye wamedumu muda mrefu kwenye mahusiano yao bila ya watu wengi kufahamu.

Tazama video hiyo hapa chini.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW