Burudani

Video iliyomkosesha usingizi Kanye West kwa miezi 5 yavuja mtandaoni ikiwa haijakamilika

Rapper Kanye West amejikuta katika wakati mgumu baada ya video yake mpya aliyoihangaikia kwa muda mrefu na aliyokua anategemea kuitoa hivi karibuni kuvujishwa mtandaoni na mtu asiyejulikana ikiwa haijakamilika.

Kanyez

Kupitia akaunti yake ya twitter jana (July 9) Kanye alitoa taarifa juu ya kuvuja kwa video ya wimbo wake mpya wa “Black Skinhead” na kudai kuwa video hiyo ilikuwa haijakamilika. Kanye aliendelea kutweet kuwa yeye na Nick Night wamekuwa wakiihangaikia video hiyo kwa miezi mitano hivyo inamuuma sana kuona kitu kama hicho kinajitokeza.

Pia Kanye ameahidi kuwa video iliyokamilika ya wimbo huo itakuwa tayari ndani ya wiki au zaidi, lakini pia hakumwacha hivi hivi yeyote aliyeivujisha alimpa alichostahili “To whoever leaked the video … F*** YOU!”

Kanye tweet

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents