Burudani

Video inayomuonesha Kalapina alivyompiga Chidi Benz Maisha Club/Exclusive audio ya Nikki Mbishi kuhusu tukio

Jumapili hii kwenye ukumbi wa New Maisha Club, kulitokea ugomvi kati ya rapper Chidi Benz na Kalapina aliyekuwa na show yake pamoja na Kikosi cha Mizinga. Tukio lilitokea baada ya Chidi Benz kupanda ghafla kwenye stage na kumnyang’anya kipaza MC wa show hiyo wakati Nikki Mbishi alipokuwa kwenye stage.

https://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=2lQ_2GYg76Y

Baada ya kupanda juu, Chidi aliyekuwa amelewa alianza kuwaongelesha na kuwaimbia mashabiki waliokuwa wakimshangilia. “Naomba niongee kitu kimoja ambacho ninyi watu woote ambao mpo humu ndani mtasikiliza, au vipi, nimeingia na beibe beibe, nimeingia VIP halafu nimemuona Nikki Mbishi anachana hapa stage, Nikki njoo njoo Nikki njoo, sijui show ya nani kwasababu yako wewe nimekuona nilikuwa paleeee, nimepita nimekuja hapa nimekuona mdogo wangu, sasa nini sasa, piga keleleeee,” alisikika akisema Chidi huku watu wakimshangilia na baadaye microphone kuzimwa.

Baadaye Kalapina alipanda kwenye stage na kuchukua microphone, “Oii ambaye hahusiki na show ashuke,” alisema Kalapina na kumfuata Chidi kisha kumpiga na kumwangusha chini. “Ninyi mnamwachia mtoto m*** apande kwenye stage,” alisema Kalapina wakati huo Chidi Benz aliyekuwa anataka kurudi tena kwenye stage kupigana akiwa ameshikiliwa na watu wa ulinzi.

Bongo5 imezungumza na Nikki Mbishi anayesimulia tukio zima na aliyesema kuwa Chidi alipanda jukwaani kushow love kwake japo hakupanda muda muafaka na unaotakiwa.

Msikilize Nikki Mbishi hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents