Technology

Video: Infinix kuipamba Valentine kwa uzinduzi wa Duka la kisasa- Infinix Smart Hub

Katika kusherehekea sikukuu ya Wapendanao, Kampuni ya Simu Infinix Mobile Tanzania imezindua rasmi Duka Jipya maarufu kama ‘INFINIX SMART HUB’, lililopo China Plaza Karia Koo. Hili ni duka la pili kuzinduliwa na Kampuni hiyo huku lengo kuu ni kuwafikia wateja wake kwa urahisi zaidi.

Katika uzinduzi huo Afisa wa Mahusiano wa Kampuni ya Simu ya Infinix, Aisha Karupa amevieleza vyombo vya habari kuwa ”Infinix imejipanga vizuri katika kutoa huduma iliyo bora zaidi kwa wateja wetu wa maeneo mbalimbali pasipo kuwa na hofu ya kutofikia kwa uharaka zaidi na katika kuhakikisha wanafanikiwa katika hilo ‘Infinix Smart Hub’ itakuwa ikitoa huduma kwa siku saba za kila wiki kuanzia Jumatatu hadi Jumapili kuanzia Saa 9:00 asubuhi hadi saa 11:30 jioni.”

Aisha Karupa amewashukuru Watanzania kwa kuzipokea bidhaa za Infinix na kuwa wateja wazuri kwao, ” Kwa mapenzi yenu tutaendelea kutanua wigo ili kuhakikisha mnapata huduma stahiki kama vile simu na bidhaa nyingine za Infinix zenye ubora zaidi zikiwa chini ya ‘Warranty’ ya mwaka mmoja na mwezi mmoja pamoja na elimu ya bure kuhusiana na utunzaji na utumiaji wa simu za Infinix kwa muda mrefu pasipo kuwaletea shida ya aina yoyote.”

Kwa upande wake Meneja wa Masoko, Saiphone Asajile ameeleza machcahe kuhusiana na mauzo ya Infinix tangu kuingia kwake rasmi Tanzania mwaka 2018 na nini Watanzania wetegemee kutoka Infinix hasa kwa kipindi hiki cha Valentine.

”Watanzania wameonesha upendo wa hali ya juu sana kwetu hadi kufikia hatua ya kuzindua duka la pili la kisasa sio hatua ndogo, kwani kuna Kampuni nyingi za simu tumezikuta lakini hawajafanikiwa kufanya hili tunalolifanya Infinix, hiki ni kiashirio tosha Infinix imeliteka soko la simu kwa asilimia kubwa, lakini vile vile katika kuendeleza upendo kama ilivyo kawaida yetu katika Msimu huu wa Valentine, Infilix inakupa Ofa ya 10%, Infinix gift package chakula cha Usiku kwa wewe na Umpendaye katika Restaurant ya kisasa.”

Uzinduzi huo ulishamirishwa na michezo mbalimbali pamoja na muziki wa Live band na kuufanya uwe wa kipekee.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents