Burudani

Video: Instagram bure kutoka Vodacom ni mkombozi – Vanessa Mdee

Msanii wa muziki Vanessa Mdee aka V Money amefurahishwa na hatua ya mtandao wa simu nchini, Vodacom Tanzania kuanzisha huduma ya Instagram bure ambayo itawafanya watumiaji wa mtandao huo kutumia huduma hiyo bila malipo.

Vanessa mdee

Mtandao huo umezindua hiyo Jumamosi hii Mlimani City Jijini Dar Es Salaam mbele ya waandishi wa habari pamoja na wadau waliojitokeza kushuhudia tukio hilo la kihistoria nchini Tanzania.

Akiongea na Bongo5 Vanessa Mdee muda mchache baada ya uzinguzi huo, alisema Instagram bure kutoka Vodacom itawasaidia mashabiki wake kufutilia muziki wake pamoja na wasanii wote.

“Binafsi niliachia albamu yangu mpya ‘Money Monday’ kwa njia ya mtandao, muziki sasa tunauuza kwa njia ya mtandao, kwahiyo ujio wa instagram bure kutoka Vodacome kwa muziki wangu kuna faida kubwa sana, mashabiki wangu watapata fursa ya kufuatilia muziki wangu kwa ukaribu zaidi kwa sababu Instagram ndio kila kitu katika maisha ya wasanii,” alisema Vanessa

Aliongeza, “Hata mimi naifurahia hii huduma kwa sababu nikinunua kifurushi cha vodacome kuanzia cha tsh 1000 unapata huduma ya Instagram bure kwa muda ambao umenunua kifurushi, ukinunua kifurushi cha wiki basi bure itakuwa ni wiki. Na nimesikia kama nikinunua kifurushi cha pinduapindua utapata ofa kubwa zaidi ya bure, kwahiyo mimi binafsi hii huduma imeifurahia kwa sababu mimi ni mtumiaji wa muda voda wa muda mrefu,”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents