Videos

Video: Kajala adai hakuwa akimpa muda mama yake kabla ya kwenda jela na kumfanya alie mara nyingi

Muigizaji wa filamu nchini, Kajala Masanja amesema kabla ya kwenda jela, alikuwa amekumbwa na maisha ya starehe na kujirusha kiasi cha kumnyima muda mama yake mzazi aliyekuwa akimhitaji hata kwa kuongea naye tu jambo analosema lilimliza mama yake mara nyingi.

Akiongea kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV jana usiku (April 16), Kajala alisema baada ya kukaa jela ndipo alipofunguka na kugundua umuhimu wa mama yake na jinsi anavyompenda.

“Mimi mama yangu ananipenda sana, sana, hata kuna kipindi ambacho alikuwa ananihitaji kukaa na mimi kuongea na mimi, lakini mimi nilikuwa nawaza tu mambo ya kwenda out na nini, simpi ile chance ya kukaa na mimi kuongea,” alisema Kajala.

“Lakini nilivyokaa gerezani nikaja kujua kwamba mama yangu alikuwa ananihitaji halafu mimi namkimbia, yaani nikawa najutia sana, kwani nilikuwa simpi mama yangu ile nafasi nikae naye! Kumbe nilikuwa namuumiza, akikaa peke yake analia, kwahiyo nilipokaa gerezani ndio nikajua kwamba mama yangu alikuwa anaumia sana, kwahiyo nikamwambia mama nisamehe na naahidi nitabadilika.”

Kwa upande mwingine Kajala alisema kwa sasa anatamani kusafiri kwenda mbali kwa muda kwakuwa bado hayuko sawa.

“Nachotamani ni kusafiri, yaani niende tu nikapumzike sehemu nisionane na watu wengi kwanza then baadaye nikirudi maisha yaendelee. Najiona si kama Kajala yule niliyekuwepo. Kuna muda nakuwa sitaki hata kuonana na watu, yaani bado siko sawa.”

Alisema kama angekuwa na uwezo kwa sasa angetafuta shule asome na hata ikiwezekana aajiriwe ili afanye kitu tofauti.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents