AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Video: Kanye West aweka wazi sababu za kuanguka jukwaani kwenye ziara yake ya Saint Pablo

Kanye West bado anaendelea kuteka vichwa vya habari kwa stori zake za kusisimua tena zikikuacha ubaki na kicheko kikubwa kutokana na vimbwanga vyake.

Rapper huyo ameweka wazi sababu zilizomfanya kuanguka jukwaani na kukimbizwa hospitali Novemba mwaka 2016 wakati wa show ya ziara yake ya Saint Pablo.

Akiongea na mtandao wa TMZ, Yeezy amesema kuwa alifanyiwa upasuaji (Surgery) wa ndani ili kupunguza unene na kutengeneza muonekano mzuri wa mwili wake.

“Nilifanyiwa Upasuaji na kutengeneza mwili wangu, sikutaka muanze kuniita Kibonge kama mlivyokuwa mkimuita Rob,” amesema Kanye.

Baada ya kukamilika kwa upasuaji huo, Kanye alipewa dawa aina ya Opioids kwa ajili ya kutumia lakini zilimuathiri na kumsababishia uchovu mkubwa kutokana na kufanya kazi nyingi.

Kanye West alilazimika kukatisha show zilizokuwa zimesalia na hivyo inadaiwa kuwa ilimsababishia hasara ya zaidi ya kiasi cha dola milioni 10.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW