Burudani

Video: Kanye West azungumzia mambo usiyoyafahamu kuhusu yeye, Kim Kardashian na mwanao North West

Huwa ni nadra sana kuliona tabasamu la Kanye West, lakini imedhihirika kuwa mapenzi yake kwa mpenzi wake Kim Kardashian na mwanao North West ndio ufunguo pekee wa tabasamu hilo.

The Kris Jenna Show / Kanye West

Pia inawezekana hujawahi kumuona Kanye akiwa ‘emotional’ kama alivyokuwa wakati wa Interview aliyofanyiwa na mkwe wake Kris Jenner iliyoruka jana. Kanye alikubali kuwa yeye ni mtu mwenye aibu na mwoga hasa anapokuwa mbele za watu tofauti na anapokuwa jukwaani.

Hisia za Kanye ambaye alikuwa na aibu flani zilikua zinajionesha hata katika mahojiano hayo hasa wakati alipokuwa akiulizwa kuhusu Kim Kardashian na North. Kanye alikuwa anachezesha mguu, anachezea vidole (zile ishara za aibu) lakini pia alikuwa na nidhamu ya kufa mtu mbele ya mkwe.

North west
North West

Kati ya vitu alivyovizungumzia kuhusu Kim ni jinsi walivyokutana na kusema alianza kumpenda Kim kabla hawajakutana so it was love at first sight. Katika Interview hiyo ndiyo Kanye alionesha picha ya mwanae North kwa mara ya kwanza.

Kris alimuuliza pia kama anapenda North naye aje kuwa rapper kama yeye, Kanye alisema atampatia fursa ya kujenga uwezo katika vitu tofauti na kisha kumuacha North mwenyewe aje kuamua kile atakachokuwa anaweza zaidi kukifanya na kuwa wao watamsupport katika chochote atakachoamua kufanya.

“Im gonna give her the opportunity to develop her different skills set, and then decide you know what she likes to do the best….we will just give the support and let her follow what she loves the most”.

Tazama mahojiano yote hapa

http://youtu.be/GXczHd4XvwU

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents