Michezo

Video: Kikosi cha Yanga SC kitakuwa na mabadiliko dhidi ya URA – Nsajigwa

Kocha msaidizi wa klabu ya Yanga, Shadrack Nsajigwa amekiri timu ya URA ipo vizuri na inacheza kitimu zaidi hivyo upo uwezekano wa kubadili kikosi chao ili kuhakikisha wanashinda katika mchezo wao wa nusu fainali wa Kombe la Mapinduzi.

 

URA wanacheza vizuri, kitimu na kwa ushirikiano mkubwa, tumejipanga na kama unavyoona tumefanya mazoezi ya mwisho na kunauwezekano hata mechi yetu inayokuja kukawa na mabadiliko ndani ya kikosi.

Wakati kikosi cha klabu ya Yanga kikijipanga kujitupa Uwanjani kuikabili URA ya Uganda, wanarambaramba Azam FC wao watakuwa na kibarua kizito cha kuikabili timu ya Singida United ambayo katika mchezo wake wa mwisho ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Yanga SC.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents