Michezo

Video: ‘Kila kitu tunaanza sisi, ubingwa, Rais kukabidhi kombe, kuvaa viatu, kupanda ndege’ Manara

Hafisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara amesema kuwa timu yake ndiyo inayoanza kila kitu kwenye nchii ikiwemo kutwaa ubingwa wakati inaanzishwa ligi, Rais kukabidhi kombe kwamara ya kwanza anaanza kwao, kupanda ndege, kuvaa viatu na kilakitu ameyasema hayo mapema hii leo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliyo hitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwenye ofisi zake zilizopo Ilala.

Kama timu tumejipanga kama alivyosema Mkuu wa Mkoa, mpaka sasa hivi tumechukua ubingwa bila kufungwa lengo la pili ni kumaliza ligi bila kufungwa tunajua kwenye mpira lolote linawezakana lakini sisi tunataka kuweka rekodi.

Rekodi ambayo itadumu na itaendelea kudumu kama ambazo nyengine tumeziweka, tunawaomba sana mashabiki wetu kiingilio kimeshushwa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF na Bodi ya Ligi wamekubaliana na maombi yetu kiingilio ni shilingi elfu mbili (Tsh 2000) kwa mzunguko na viti rangi ya Chungwa, hatutarajii kuona mtu akakosa lakini pia VIP B ni shilingi elfu 10000 na VIP A elfu 15000.

Tunaomba kila mshabiki aje ubingwa huu tumeukosa kwa miaka mitano kwa shabiki wa Simba sidhani kama atakaa nyumbani lakini pia tuvae jezi za ubingwa wa Simba ambazo zinauzwa kwa shilingi 15000 tuje kibingwa sisi ni Mabinwa wa nchi tumpe heshima Rais Magufuli.

Yanasemwa kwanini anapata mualiko Mkuu wa Mkoa, hapana Simba ni bingwa heshima hii amepata yeye

Kama Rais amekubali wito wa kuja kwenye mechi ya Simba ipo siku atakwenda kwenye mechi ya watani, lazima kuwe na mwanzo leo kafanya kwetu ipo siku atakuja kwa timu nyingine, tujae uwanjani kumuunga mkono kwakuwa ni kwa mara yake ya kwanza kuja kwenye mechi ya ligi kuu.

Bahati nzuri Simba ndiyo kilakitu inaanza kwenye nchi hii, ubingwa tulianza kuchukua sisi, Rais wa kwanza kutukabizi kombe sisi, kila kitu Simba tu mapaka ndege tumeanza kupanda sisi, viatu tumeanza kuvaa sisi kila kitu tunaanza sisi ni utaratibu ambao Mungu tu anatupa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents