Habari

Video: Kiongozi mkubwa ACT – Wazalendo akimbilia CCM

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni na Uchaguzi Taifa wa Chama Cha ACT Wazalendo, Samson Mwigamba ametangaza kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) baada ya kujiuzulu uongozi wa chama hicho siku za hivi karibuni.

Akizungumza na waandishi wa habari, Ndugu Mwigamba amesema kuwa CCM ya sasa ndicho chama kinachoakisi kwa karibu itikadi,falsafa na sera za ACT – Wazalendo.

“Baada ya kutangaza kujivua uongozi baadhi ya viongozi wa ndani ya chama waligeuka vichaa wakinitukana kila aina ya matusi. Cha ajabu hata wale wanaofahamu na kuitetea misingi ya chama walitukanwa na viongozi wakiwepo na wamekaa kimya, hii inaonyesha wamewatuma,” amesema Mwigamba.

Aidha Mwigamba amesema kuwa baada ya kutafakari ameamuwa kujiunga CCM kwa sababu “CCM ya sasa ndicho chama kinachoakisi kwa karibu itikadi,falsafa na sera za ACT – Wazalendo ambazo mimi na wenzangu tulishiriki kuziasisi, Kujiunga katika mapambano dhidi ya rushwa ba ufisadi, kujitenga na upinzani unaokerwa na mafanikio ya serikali

Jana Katibu Muenezi wa Chama hicho alisema kuwa Ijumaa hii watakaa kikao kujadili suala la kiongozi huyo kujiuzulu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents