Habari

VIDEO: Kuongoza nchi kazi ngumu sana, nawaza mzee Kikwete, Mkapa na Mwinyi waliwezaje kwa miaka 10?- Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Magufuli amesema kazi ya kuongoza nchi ni nzito yenye kuhitaji umakini wa hali ya juu na akawaomba waumini wa dini zote nchiniwasiache kuiombea serikali.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Jumapili Novemba 4, 2018 wakati akitoa salamu zake kwenye maadhimisho ya miaka 150 ya Ukatoliki Tanzania Bara yaliyofanyika Bagamoyo mkoani Pwani.

Nahitaji maombi sana kutoka kwenu na hata maoni, changamoto za kazi hizi ni ngumu sana nawaza hivi hawa wazee walionitangulia kina Mzee Kikwete (Jakaya), Mkapa (Benjamin) na Mwinyi (Ali Hassan)  walimalizaje miaka 10, ni kazi nzito inahitaji maombi kwelikweli,” amesema Rais Magufuli.

Kwa upande mwingine Rais Magufuli amewaomba Waumini wote waiombee Serikali kwani kuongoza nchi sio kazi rahisi.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents