HabariUncategorized

Video: Kwanini serikali imelifungia gazeti la MwanaHalisi?, Dkt Abbas aeleza

Baada ya Serikali kusitisha uchapishaji na usambazaji na gazeti la kila wiki la MwanaHalisi kwa kipindi cha miezi 24 kwa kiuka miiko na maadili ya kiuandishi ikiwa ni pamoja na kuandika habari za uongo. Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari- MAELEZO – Dkt Hassan Abbasi aweka wazi.

Akizungumza na wanahabari, Mkurugenzi Mkuu wa Habari – Maelezo na Msemaji Mkuu wa serikali, Dkt Hassan Abbas amesema kuwa Serikali imekuwa ikiliita gazeti hilo mara kwa mara kwaajili ya kuhitaji kujua kwanini wamekuwa wakiandika habari za uongo na za kichochezi wamekuwa wakijitetea na kusamahewa na mwisho wa siku wamekuwa wakirudia makosa yaleyale. Kwahiyo serikali imelifungia gazeti hilo kwa muda wa miaka miwili kujitafakari.

“Gazeti la MwanaHalisi lilionywa sana na kutakiwa kubadilika lakini mara zote waliomba radhi na kuendelea na makosa yake yale. Tumetumia muda mrefu kuwaonya tukiamini ipo siku wataacha kufanya kitu kinachofanana na uandishi wa habari na kufanya uandishi wa habari,” alisema Dkt Abbas.

Aidha Dkt Abbas alisema uamuzi wa kulifungia MwanaHalisi umechukuliwa kwa mujibu wa kifungu cha 59 cha Sheria ya Huduma za Habari Na. 12, 2016.

Soma taarifa kamili:

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents