Burudani

Video: Lil’ Kim kutoka na Nature

Mwanamuziki wa Kimataifa kutoka nchini Marekani, Lil Kim ambaye alitua hapa bongo kwa onesho lake moja ndani ya tamasha la Fiesta Jipanguse lililofanyika jana katika viwanja vya Lidaz Club, Kinondoni jijini Dar na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu kutoka sehemu mbalimbali, ametamka wazi na kuahidi leo jioni kuwa atarekodi baadhi ya nyimbo na msanii nguli wa Bongofleva Sir Juma Nature.

Lil Kim aliweka bayana hilo jioni ya leo alipokuwa akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga.Amesema amefurahishwa sana na ushirikiano mkubwa alioupata kutoka kwa Juma Nature na Watanzania kwa ujumla,hivyo kufuatia ushiikiano huo LiliKim ameahidi kurekodi baadhi ya nyimbo na Juma Nature zikiwemo remix za Mwanadada huyo mwenye manjonjo kibao awapo jukwaani.

Kama vile haitoshi, na kwa kulithibitisha alisemalo Lil Kim amechukua nyimbo kadhaa za Juma Nature na kuondoka nazo kwa ajili ya kuzifanyia kazi kwa namna moja ama nyingine,aidha Lil Kim pia ameukubali sana muziki wa Kitanzania na namna Watanzania wanavyowakubali wasanii wao tofauti na sehemu nyingine.

Lili Kim na crew yake kabla ya kukwea pipa na kurejea kwao, walipelekwa Kijiji cha Makumbusho na kujionea mambo kadha wa kadha zikiwemo nyumba za makabila mbalimbali ya Kitanzania.

Watch a video clip from Lil’ Kim’s performance in Dar es Salaam Tanzania along side Sir Juma Nature

{youtube}9P4mazemkTs{/youtube}

More videos to follow soon..stay tuned!

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents