Burudani

Video: Lil Wayne na Justin Bieber walivyomsindikiza Floyd Mayweather ulingoni juzi

Jumamosi usiku, Lil Wayne na Justin Bieber walimsindikiza mshkaji wao Floyd Mayweather, Jr. ulingoni kupambana na Saul Canelo Alvarez jijini Las Vegas.

http://www.youtube.com/watch?v=K5FH7kS6ea8

Akiwa kifua wazi, Weezy alitumbuiza wimbo wake ‘A Milli’ wakati Bieber aliyekuwa na miwani nyeusi akitembea kwa mbwembwe wakati wakiingia kwenye ulingo wa MGM Grand Garden Arena.

Baada ya pambano hilo, Bieber aliuponda uamuzi wa jaji mmoja aliyetoa pointi sare na kuandika: “Who calls a draw? That guy was watching the wrong fight. @FloydMayweather is the greatest. #MoneyTeam still #undefeated.”

Naye Weezy alimpongeza Mayweather, “Proud to be a part of the legacy of one of the greatest athletes that ever lived. & that’s the legacy of the great Floyd “$” Mayweather TMT.”

Bieber na Wayne walianza kuwa marafiki na Mayweather mwaka jana baada ya bondia huyo kumshinda Miguel Cotto.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents