Michezo

Video: Lionel Messi aukwea Mlima Kilimanjaro kimya kimya kufanya tangazo la Turkish Airlines?

Ni kweli mchezaji wa Club ya Barcelona, Lionel Andrés Messi mwishoni mwa mwaka 2013 alitua Tanzania kimya kimya kufanya tangazo la Turkish Airlines kwenye Mlima Kilimanjaro? Ni ngumu kuthibitisha hilo lakini kwa mujibu wa tangazo hilo, Messi anaonekana akijipiga picha juu ya Mlima huo mrefu barani Afrika.

6812765_orig

Idea ya tangazo hilo ni kuwa Messi na mchezaji wa mpira wa kikapu wa timu ya Los Angeles Lakers, Kobe Bryant wanashindana kupiga picha bora zaidi aina ya selfie. Tangazo linaanza kwa Messi kumtumia picha Kobe yake mwenyewe akiwa mbele ya kanisa la Saint Basil’s Cathedral mjini Moscow.

1316388_orig

Kobe naye anajibu mapigo kwa kwenda kwenye kuta maarufu za China (The Great Wall of China) na mashindano yanaendelea hadi kumfanya Messi aje kuchukua selfie kwenye mlima Kilimanjaro, huku maeneo yote hayo yakifikika na ndege za Turkish Airlines. Mwisho Messi anajipiga picha akiwa Sultanahmet Square mjini Istanbul, na kuja kugunduaa nyuma yake alikuwepo Kobe aliyetokea pia kwenye picha yake.

2130077_orig

8004664_orig

9903675_orig

Tazama tangazo lao hilo ambalo tangu liwekwe December 3 limeshaangalia kwa zaidi ya mara milioni 135.

http://youtu.be/jhFqSlvbKAM

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents