Habari

Video: Mahojiano na Emanuel Austin (dancer wa kimataifa) aishiye Ujerumani

Mwalimu wa dance, Mtanzania aishiye nchini Ujerumani, Emanuel Austin, wiki hii ametua jijini Dar es Salaam, ambapo amekuja kwa shughuli za msaada na kufundisha watoto kucheza muziki.

Mwalimu huyo aliyeambatana na mchumba wake Lara, alikuja kwenye studio za Bongo5 kufanya interview na kuzungumza kuhusiana na shule yao waliyoianzisha nchini Ujerumani kufundisha kucheza muziki na madhumuni ya safari yake ya Dar.

Historia yake fupi

Emanuel alizaliwa tarehe 27.10.1990 jijini Dar es Saalam lakini amekuwa akiishi nchini Ujerumani na wazazi wake kuanzia mwaka 1996. Akiwa na umri mdogo alikuwa akipenda kuigiliza namna wanavyocheza wasanii kama Michael Jackson na kujikuta akipenda zaidi kucheza hip-hop.

Mwaka 2006 alishinda shindano la vipaji vya kucheza huko Hanau, Ujerumani. Mwaka 2008, alianza kufundisha masomo ya kucheza na kujikita zaidi katika hip hop, michezo ya watoto na Salsa Cubana. Pia amekuwa akifundisha kucheza Merengue na Bachata.

Mpaka sasa, Emanuel Austin anafanya kazi kwenye shule kubwa ya dance nchini Ujerumani na ameshacheza kwaajili ya mastaa Don Omar, Jason Derulo na Usher huku pia akifanya kazi kama model.

Mfahamu zaidi kwa kutembelea ukurasa wake wa Facebook hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents