Video: Major Lazer wawakutanisha uso kwa uso mastaa wakubwa Afrika

Kundi la watayarishaji wa muziki na Madj maarufu wa Marekani, Major Lazer limeachia video ya wimbo wao “Particula” iliyofanyika katika jiji la Johannesburg, Afrika Kusini na kuongozwa na mtayarishaji wa filamu, Adriaan Louw.

Kwenye video hii yenye muonekano wa Kiafrika, wanaonekana mastaa wa Afrika Kusini, Dj Maphorisa na Nasty C, rapper wa Nigeria Ice Prince, na msanii wa Marekani mwenye asili ya Nigeria, Jidenna.

“Particula” inapatikana kwenye EP mpya ya Major Lazer iitwayo Know No Better ambayo waliichia kwa kushtukiza mapema mwaka huu na kupokelewa kwa sifa nyingi.

Nyimbo zinazopatikana kwenye EP hiyo zimetazamwa kwa kiasi kikubwa mtandaoni ambapo wimbo uitwao “Sua Cara” waliowashirikisha mastaa wa Brazil, Anitta na Pabllo Vittar ni moja ya video zilizotazamwa zaidi Youtube kwa zaidi ya mara milioni 217 hadi sasa.

EP hiyo imekusanya ladha za dunia nzima na imeshawishiwa na safari yao huko Pakistan, Cuba, America Kusini na Afrika huku wakiongezea ladha za Carribean.

Know No Better imekusanya wasanii mashuhuri kuanzia Machel Montano, Busy Signal, Sean Paul, Konshens, J Balvin na wengine huku watayarishaji kama Jr. Blender, Boaz van de Beatz na King Henry wakihusika pia.

Know No Better inafuata mafanikio ya ngoma za Major Lazer zikiwemo “Run Up” waliowashirikisha PARTYNEXTDOOR na Nicki Minaj, “Cold Water” waliowashirikisha Justin Bieber na MØ pamoja na “Lean On” wakiwa na DJ Snake na kumshirikisha MØ, ambao umekuwa moja ya nyimbo zilizofanikiwa katika muda wote.

Major Lazer kwa sasa wanafanya ziara dunia nzima.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW