Michezo

Video: Manara acharuka baada ya shabiki wa Simba kudundwa na mashabiki wa Yanga ‘kwahili siwaachi’

Video: Manara acharuka baada ya shabiki wa Simba kudundwa na mashabiki wa Yanga 'kwahili siwaachi'

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Simba, Haji Manara ameonekana kukerwa na kitendo kilichofanywa na baadhi ya mashabiki wa Yanga kumvamia na kumfanyia vurugu mtu mmoja aliyesadikika kuwa shabiki wa Simba.

Manara ameyaeleza hayo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram huku akiweka na kipande cha video kinachoonyesha tukio hilo.

 

Tuna aina ya watu washamba sana na hawa ndio aina ya watu ambao tunapaswa tuwalaani..hv why baadhi ya wanayanga wanajiona wao ndio wenye haki nchi hii peke yao?kutucharura wafanye wao ikifanya Simba ni kosa au ushenzi wa kumpiga shabiki wetu..hv akifa huyo mtu?hili siwaachi soon mtasikia..mapimbi kama hao mm ndio Mchungaji wao..ntawatia adabu!! Mijitu imetoka kwenu Manyenza huko mnatuletea ujinga!! Mnavunja hadhi ya klabu yenu na inaonekana ni klabu iliyofuga watu wahuni.

Hayo yamekuja baada ya shabiki huyo wa Simba aliyevalia jezi ya timu hiyo kupita kwenye jukwaa lililozoeleka kuwa la mtani wake Yanga wakati wa mchezo wa Wanajangwani hao.

Related Articles

3 Comments

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents