Michezo

Video: Maneno ya nahodha Nadiri Haroub ‘Cannavaro’ baada ya mazoezi ya mwisho huko Shelisheli

Mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya mwisho katika uwanja wa Stade Linite huko Victoria Shelisheli nahodha wa mabingwa wa tetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara Yanga SC, Nadiri Haroub ‘Cannavaro’ amesema kuwa kila mchezaji anahamu ya kucheza mechi ya kesho na kuwataka Watanzania kuwaombea ili kuweza kuchomoza na ushindi.

Tunamshukuru Mungu tumemamaliza salama mazoezi na kila mchezaji anahamu ya kucheza mechi ya kesho na tunawaomba watanzania kwa ujumla wana East Afrika watuombee duwa ili tuweze kufanya vizuri na sisi ahadi yetu ni kuhakikisha tunafanya vizuri ili tuweze kuendelea katika mashindano haya makubwa.

Tulipata goli moja lakini siyo dogo inamaana tukipata lingine tunakuwa tupo mbali kwahiyo tunachotakiwa sisi ni kucheza tu kwa tahadhari ili tuweze kufanya vizuri katika mchezo wa kesho na morali ya wachezaji ipo vizuri na tupo tayari.

Mabingwa hao wa Tanzania Bara wanajiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya St Louis hapo kesho siku ya Jumatano huku wakiwa na faida ya ushindi wa nyumbani wa bao 1-0.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents