Michezo

Video: Masau Bwire aapa kuiuwa Simba kesho ‘Tunakuja nakamfumo tunakaita Noto, msikose kuja kushuhudia’

Msemaji machachari wa klabu ya Ruvu Shooting, Masau Bwire ametamba kuwa timu yake itaifunga Simba SC kwenye mchezo wao wa kesho siku ya Jumapili utakaopigwa majira ya saa 1:00 usiku kwa mfumo mpya unaoitwa ‘Noto’.

Masau ameyasema hayo kupitia Azam tv, huku akijinasbu kuwa lengo lao ni kuleta mabadiliko ya soka la Tanzania na kujaribu kuondoa fikra ndani ya vichwa vya Watanzania kwamba mpira wa miguu wa nchi hii ni wa Simba na Yanga.

”Tunakuja na kamfumo fulani ndani ya Papasa Squared tunakaita NOTO sasa Watanzania watajua nini maana ya Noto,” amesema Masau Bwire.

Masau Bwire ameongeza ”Siku ya Jumapili niwaombe tu Watanzania wasikose kufika sisi lengo letu ni kuleta mabadiliko ya soka la Tanzania na kujaribu kuondoa fikra ndani ya vichwa vya Watanzania kwamba mpira wa miguu wa nchi hii ni wa Simba na Yanga.”

”Kidogo sasa hivi Azam wanakuja kuja, Singida walikuwa wanapewa kipaumbele hao tayari tumeshawashukhulikia wala hatuna shida nao tena tunawatazama hawa watatu waliyobaki.”

Masau ameyasema hayo kupitia Azam tv, huku akijinasbu kuwa lengo lao ni kuleta mabadiliko ya soka la Tanzania na kujaribu kuondoa frika ndani ya vichwa vya Watanzania kwamba mpira wa miguu wa nchi hii ni wa Simba na Yanga.

https://www.instagram.com/p/Bpbt1-xBACJ/?taken-by=azamtvtz

Ruvu Shooting itaingia kwenye mchezo huo wakati ikitoka kupata ushindi mnono wa mabao 3 – 0 dhidi ya moja kati ya timu ngumu Singida United wakati Simba ikitoka na ushindi mnono wa bao 5 – 1 mbele ya vijana Alliance FC.

https://www.instagram.com/p/BpXC7F4h3tW/?taken-by=ruvushootingfootballltd

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents