Burudani

Video: Max Rioba hakuwa serious na kazi – Young Dee

Msanii wa muziki wa hip hop, Young Dee kutoka King Cash, amedai kwa muda mfupi aliokaa ndani ya label yake mpya amegundua menejimenti yake ya zamani, ‘MDB’ ya Max Rioba haikuwa serious na kazi.

Rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo Bongo Bahati Mbaya (BBM), ameiambia Bongo5 kuwa kwa sasa amekutana na watu sahihi ambao wataupeleka mbele muziki wake.

“Utofauti uliopo kati ya ‘MDB’ na King Cash ni u-serious wa kazi. Kwa sasa nafanya kazi na watu ambao wanaijua kazi wanayoifanya na niwazoefu wa kazi,” alisema Young Dee.

Aliongeza,“Unajua kufanya kazi na watu wanaojua kazi ni toafuti na watu wanaojifunza kazi, suala linakuja kwenye uzoefu,”

Rapa huyo amedai ndani ya muda mfupi ameaona kuna dalili za muziki wake kufanya vizuri zaidi kimataifa tofauti na awali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents