Habari

Video: Mazishi ya Ivan yafanya kufuru Uganda

Ivan Ssemwanga ambaye alifariki wiki iliyopita alizikwa jana jioni kijijini kwao Nakalilo katika wilaya ya Kayunga nchini Uganda, lakini msiba huo ulionekana kuvunja rekodi kutokana na waliokuwa watu wa karibu wa marehemu kufanya vitu vilivyowashangaza wengi.

Msiba huo ulihudhuriwa na watu kibao wakiwemo mastaa wa Uganda Jose Chameleone, Bobi Wine, Weasel Manizo na wengine.


Jose Chameleone akiwa katika msiba wa Ivan

Lakini kubwa zaidi linalozungumziwa katika mazishi hayo ni kipindi ambacho watu ambao walionekana kuvalia nguo nyeusi walimwaga pombe, fedha katika kaburi la marehemu Ivan kitendo ambacho hakijazoeleka kikawaida.

Tazama video hiyo hapa chini.

https://youtu.be/nNtSSzHPZjY

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents