Habari

Video: Mbunge Nassari asifia utendaji kazi wa serikali ya awamu ya tano

Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (CHADEMA) ameipongeza na kuisifu serikali ya Awamu ya Tano kwa jitihada kubwa inazofanya katika kuwaletea wananchi maendeleo bila kujali maeneo wanakotoka kote nchini.

Nassari ametoa pongezi hizo jana mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyekuwa katika majumuisho ya ziara yake ya siku 10 ya kikazi mkoani Arusha. Mbunge huyo aliyelazimika kuja nchini kwa dharura akitokea masomoni nchini Uingereza ili kumuwahi Waziri Mkuu, alisema ameridhishwa na hatua za utatuzi wa migogoro ya ardhi zinazochukuliwa na Serikali.

Mbunge huyo alimuambia waziri mkuu kuwa,”nimefarijika sana kwa feedback ambayo nimeipata kutoka kwa waheshimiwa wabunge wenzangu kwa majibu yao yaliyopita kwanza nishukuru kwa commitment ya serikali ya awamu ya tano ambayo imeonyesha kwa lile lililopo kwa kuwafikia wananchi na sisi kama wawakilishi wa wanachi hiyo imekuwa kiu yetu kwa siku nyingi, na hii ndio dhamira ya serikali ya awamu ya tano kwa kutuhakikishia feedback tunayoipeleka kwa wananchi wetu inakuwa feedback nzuri ya mahusiano na ushirikiano,” alisema Nassari.

https://youtu.be/DiihynMsTrs

Waziri Mkuu juzi alipofanya ziara katika wilaya ya Arumeru alisema serikali itawanyang’anya ardhi wamiliki wote wenye mashamba makubwa wilayani humo ambao hawajayaendeleza kwa sababu wamekiuka mkataba wa umiliki.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents