Video: Meet Linah

 

Msanii wa kike mwenye umri mdogo kuliko wasanii wote wa kike hapa nchini Linah (Estalina Sanga)  ambaye anakuja juu sana aliongea na Bongo5 na kueleza mpango wa kwenda kusomea mambo ya production.

Linah alisema hayo katika Studio ya Ndoma Records iliyopo jijini Dar es Salaam alipokwa akirekodi albam yake ya kwanza inayotarajia kuzinduliwa tarehe 8 mwezi wa 12 itakayokwenda kwa jina la  Atatamani.

Msanii huyu aliongezea kuwa  anapenda kwenda kuseomea fani ya production, kwani itamsaidia  katika  kazi yake ya muziki  maana maisha yake yote ni muziki na  atakuwa amesomea kitu ambacho kinaendana na kipaji chake.

Linah ambaye ameimba nyimbo ya Atataman, Bora nikimbie, ambazo nyimbo zake zinapigwa na kuchezwa karibia vituo vyote vya redio na television, ameshirikisha na Barnaba katika wimbo wa wrong number ambapo Linah alionekana akifanya vizuri katika wimbo huu hizi ni baadhi ya nyimbo ambazo masanii huyu ametoa.

{mmp3}lina_bora_nikimbie.mp3{/mmp3}

{hwdvs-player}id=1237|tpl=playeronly{/hwdvs-player}

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW