Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Video: Mfahamu bingwa huyu wa kuchezea pikipiki duniani

Je unamfahamu Toni Bou? Huyu ni kijana mwenye umri wa miaka 31 lakini ana uwezo mkubwa wa kuonyesha michezo tofauti tofauti kwa kutumia pikipiki.

Historia ya kijana huyu ni nzito maana amefanikiwa kushinda mataji makubwa tofauti tofauti duniani ya mchezo huo zaidi ya 11 mpaka sasa tangu alipoanza kucheza mchezo huo mwaka 2001 akiwa na umri wa miaka 15.

Awali bingwa huyu alikuwa akiendesha baiskeli katika mashindano mbali mbali ya watoto tangu alipokuwa na umri wa miaka nane, lakini aliachana na mchezo huo baada ya kushinda mashindano ya dunia kwa watoto kupitia mchezo huo mwaka 1999 na hapo ndipo alianza kujifunza kuchezea pikipiki.

Bingwa huyu alizaliwa katika mji wa Barcelona nchini Hispania. Tazama video ya Toni Bou akionyesha uwezo wake wa kucheza na pikipiki.

Leave a comment

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW